MRADI WA KUSAIDIA WATOTO WADOGO MANG`ULA

WALENGWA:
Watoto wadogo kuanzia miaka 3 hadi 6, hususani yatima.

JINA LA KITUO:
Mangula children caring fund
(Mfuko wa kulea watoto wa Mangula).

 

ANUANI:
S.L.P. 83
MANGULA
KILOMBERO MOROGORO
TANZANIA 255

BARUA PEPE:
john.mansur@gmail.com

KUANZISHWA MRADI:
mei 10, 2005

 

MALENGO MAHSUSI:
Shirika letu limeanzishwa rasmi hapa kijijini baada ya kuona watoto wengi sana wanabakia mitaani , wakihangaika bila ya kwenda madarasani. Badhi yao wamekosa wazazi baada ya wazazi hao kufariki na ukimwi(HIV). Au kukosa malezi mema ya familia kutokana na umaskini. Familia zao zimekuwa na kazi nyingi za shamba. Hivyo watoto wanabaki bila mlezi na kuweza kuhatarisha maisha yao kwa ujumla. Mangula ni kijiji chenye wakazi wapatao 22,000 kulingana na sensa ya mwaka 2000. Yapata theluthi moja zaidi kuwa ni idadi ya watoto umri kati ya miaka 3 hadi 6.

  • Hivyo Tukaanzisha shule ya watoto wadogo ili tuwapatie elimu ya awali. Msaada unalengwa hasa kwa watoto yatima (orphaned children).
  • Kuanzisha vituo vya michezo kwa watoto wadogo
  • Kutoa ushauri nasaha juu ya maambukizo na athari za ukimwi (HIV/AIDS).


LENGO KUU MWAKA 2006:
Kutokana na tatizo kubwa la eneo la kusomeshea watoto, shirika letu linajitahidi kwa kila hali kutafuta msaada wa kifedha ili tuweze kujenga shule ya watoto wadogo. Tutahitaji kunua shamba lenye ukubwa wa heka mbili au zaidi. Jengo la sasa linagharimu pesa nyingi kila mwezi. Watoto wanaongezeka kila siku. Tunakosa eneo la kutosha michezo kwa watoto.

Tutafuraha na kushukuru sana kama tunaweza kusaidia kujenga madarasa kwa
shule mpya.

MUNGU BARIKI KAZI ZENU.....!