MRADI WA KUSAIDIA WATOTO WADOGO MANG`ULA

WALENGWA:
Watoto wadogo kuanzia miaka 3 hadi 6, hususani yatima.

JINA LA KITUO:
Mangula children caring fund
(Mfuko wa kulea watoto wa Mangula).

 

 

 

 

    
 

 

  


 

 

 

 

ANUANI:
S.L.P. 83
MANGULA
KILOMBERO MOROGORO
TANZANIA 255

BARUA PEPE:
john.mansur@gmail.com

KUANZISHWA MRADI:
mei 10, 2005

 

HISTORIA YA MRADI WA MACHICA:

MACHICA: Neno machica linatokana na Mang’ula Children Carring fund. Ambapo kwa Tanzania makao makuu yapo Tarafa ya Mang’ula, Halmashauri ya mji wa Ifakara, mkoa wa Morogoro na anuani ni MACHICA ASSOCIATION S.L.P 83, Mang’ula, Morogoro, Tanzania.

Machica ni mradi ambao umeanzishwa kwa sababu mbalimbali kama vile, matatizo mbalimbali yanayowakabili  kaya masikini ususani yatima katika kuleta muafaka wa kupata maendeleo kwa jamii husika pasipokupata shida yoyote kupitia mradi wetu.

Hii nikutokana na serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa wito (fursa) kwa asasi za kiraia ikiwemo Machica kuanzisha huduma zake kwa lengo la kuleta maendeleo ya nchi kupitia malezi bora ambayo yataleta chachu kubwa ya maendeleo baada ya kuwalea kikamilifu makundi husika ambayo mradi yana shughulikanayo. Makundi hayo ni watoto wenye mazingira hatarishi pamoja na yatima kwa msaada mkubwa ambao tunaupata kupitia marafiki zetu mbalimbali hasa kutoka nchini ujerumani Machica ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa na malengo makuu yafuatayo.

Makundi yenye mazingira magumu kama vile yatima, ambao wanapaswa kupata faraja yakutosha kupitia msaada ya karibu ya malezi kutoka nje na ndani ya mradi.

Wanachama wanatakiwa kufanya kazi kwa pamoja kupitia ujuzi walionao ili waweze kuleta msaada mkubwa kwa yatima, walemavu pamoja na wazee. Kushirikiana na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ili kuweza kuleta mafanikio ambayo mradi imeyakusudia hasa katika kuleta ushirikiano katika vyanzo mbalimbali vya mapato ili kuweza kumudu malengo ya kuwalea makundi ambayo tumeyakusudia.

Kuunga mkono jitihada za serikali na za asasi za kiraia zenye malengo ya kuleta na kuchangia maendeleo katika Tarafa ya Mang’ula.

Kutafuta watu wanaokuja kujitolea kutoka ndani na nje ya nchi ambao wana uwezo wa kujitolea kufanya kazi katika sehemu moja au zaidi ya moja.


MAFANIKIO:

Mradi wa Machica kwa sasa unatakribani miaka 16 tukiwa na marafiki zetu kutoka nchini ujerumani.

Mradi umeweza kuwa na Mafanikio ya kuwalea watoto yatima katika mazingira ya mradi (Mabweniya mradi kwa kuwapatia huduma za msingi ikiwemo chakula, malazi, pamoja na mavazi.

Mradi umeweza kuliunga mkono suala la utunzaji mazingira kwa kutumia umeme wa nishati ya jua ambayo pia ilichangiwa na marafiki zetu kutoka nchini ujerumani.
Mradi kwa sasa umeweza kuwasaidia vijana wakike watatu katika masomo yao ya sekondari kupitia michango katika kuwapa pesa za kujikimu pamoja na taaluma. Vilevile mradi kupitia marafiki umeweza kutoa mshahara kwa watumishi wote wa taasisi ili waweze kujikimu kimaisha.

Vilevile mradi kupitia marafiki umeweza kutoa mishahara kwa watumishi wote wa taasisi ili waweze kujikimu kimaisha. 

Mradi kwa sasa umefanikiwa kuwa na watumishi kumi na moja ambapo kati ya hao nane ni wanawake na watatu ni wanaume.

Mradi unapata msaada mkubwa kutoka kwa marafiki zetu kutoka ujerumani ili kuweza kuwezesha shughuli mbalimbali ambazo mradi unazitekeleza mfano kilimo, umeme wa jua, ujenzi wa majengo ukarabati pamoja na ada za shule kwa baadhi ya watoto. 

Mpaka sasa mradi umefanikiwa kuwa na mradi wa ufugaji wa kuku, pamoja nap aka katika mradi hii itapelekea kupitia kuku kupata nyama pamoja na mayai, vilevile tutapata ulinzi mkali wa paka kwa panya wasumbufu.

Naomba kuwasilisha.

Boniface Chigwanda
Manager wa mradi